jump to navigation

Around Oldoinyo Lengai There is Life! December 21, 2010

Posted by tanzaniageologists in Uncategorized.
trackback


Tulipokuwa njiani kuelekea Oldoinyo Lengai nilikuwa najiuliza kama huko mbele tunapoenda watu wanaishi, but immediately after arriving there jibu lilikuwa wazi tu. Wapo watu wengi around ule mlima, kama sikosea kuna vijiji kama vitano hivi na kilicho karibu kabisa na mlima na chenye watu wengi ni kijiji cha Engaresero. Kina takribani watu zaidi ya 500. Jamii kubwa hapa ni wamasai watoto mpaka wazee. Kuna makabila mengine kama wairaq, wachaga nk. Kama kawaida ya sisi watanzania kila mahali ni nyumbani na wote ni ndugu, watu wa hapa ni wakarimu sana na wanamsaada mkubwa kwa wageni especially linapokuja suala la kupanda mlima au kuzunguka maeneo yaliyo karibu na mlima. Ukifika pale one day as a tourist or a geologist ulizia hawa watu wawili Bura na Tall (huyo hapo kushoto aliyekaa chini, mmasai). Hawa ni wataalamu mfano huyu tall anaweza kupanda mlima na kurudi chini na akakupita tana kabla wewe hujapanda/hujafika nusu ya mlima. Kuna Mzee anaitwa Bura (huyo hapo kati yetu kushoto anatusaidia kucollect sample), yeye anauzoefu wa takribani miaka 25 katika eneo hilo na mara ngingi watalii wakija yeye ndio huwa anaongoza msafara wa kupanda mlima. Kupanda mlima huwa ni usiku na hii ni kwa sababu maalumu, mchana hutaweza kupanda coz kuna jua kali na mlima pia due to its chemistry unareflect sana so unaumia sana macho ndipo wakaona ni vyema kupanda mlima usiku. Safari ya kupanda sio raha unatakiwa uwe shupavu na jasiri sababu wanyama kama chui ni wakawaida mlimani na unaweza ukawa umelala kwenye hema mlimani ukasikia chui anazunguka hema lako. But kama nilivyokwambia watu wa hapa ni wataalamu na wazoefu wa hawa wanyama. kabla ya kuanza wanakupa some hints kwamba tukikutana na mnyama flani unatakiwa ufanye hivi na vile na mnyama ataondoka bila kukuzuru. Masharti yao au njia zao zinasaidia coz kule mlimani hutaweza kukimbia hata 2steps coz unaweza angukia kwenye shimo na usionekane milele. Well that is it about climbinig.
Nilisema kuna maisha Oldonyo lengai ingawa kwa kupaona unaweza kusema huwezi kukaa hata 2 days, kuna vibanda na nyumba za biashara Nyama ndio chakula kikuu utakikuta pale tena mbuzi na kama nilivyokwambia mbuzi au nyama za huku kwa ujumla ni tofauti na za mijini ni nzuri sana nayo hii inachangiwa na geoological processes katika eneo hili. Bia (geological water) na soda zipo kwa sana tu na mfano wa bar zao ni hiyo hapo kulia na kama sitakosea hiyo hapo kwenye picha wakati ule ilikuwa inaitwa “Obama Grocery”. Hapo wale wa serengeti (sere/chui) mtapata tu ingawa bia inayonyweka sana na watu wa hapo ni safari , nazani hii ni sehemu nyingi za vijijini wanakunywa safari coz hata chimala mbeya nimeona hiyo pia. Usiulize ya baridi hutapata coz hata wewe wa mjini sasa hivi unaanza kukosa vya baridi, yah si huna umeme (mgawo) na mwakani wanaupandisha huo wa mgao kwa 18% so utakuwa kama watu wa Oldoinyo tu. Tena nafuu wale coz wana utaalamu wa kuzifanya ziwe baridi, huwa wanaweka kwenye maji yaliyo tulia ili zipoe kidogo. Well kama nilivyokwambia ukiwa kule ni mwendo wa nyama na kama utahitaji dawa za kienyeji zipo tu, wajamaa hawa pia ni wataalamu kwenye medications, ukisema naumwa tumbo dkk 2 umeletewa dawa na anakwambia arafiki kula hii ingawa ni ya kunywa kama maji yeye anakwambia kula ila unaelewa tu na kweli utapona. Kuna dawa za aina nyingi wenyewe wanasema. Mfano mswaki, ndulele, etc. Hawa watu wa hapa ni wema sana na wema wao hata wanyama wa porini wanaujua, ni jambo la kawaida sana kukuta mmasai anachunga ng’ombe porini na hao ng’ombe unakuta wamechanganyikana na wanyama wa porini kama nyumbu swala nk. Cheki picha hapo kwa makini ingawa sio nzuri utaona nyumbu ktk kundi la ngombe na hii ni kwa sababu wamasai hawali wanyama wa pori ingawa chakula chao kikuu ni nyama na maziwa. Sipati picha kama hii ingetokea kule uchagani coz nilishapigiwa story kwamba kuna mchaga alijikata kidole bila kujua akiwa anagombania nyama ya nyati hahaha! strange ila in kweli na alipata nyama ingawa sijui kama alipata kidole chake. OK naomba niishie hapa kwa leo coz jukumu kuu nililonalo (shule) ndilo linanicontrol. Vielen Dank!

Comments»

No comments yet — be the first.

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google photo

You are commenting using your Google account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s

%d bloggers like this: